• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping asema hakuna nguvu yoyote inayoweza kuzuia wananchi wa China kutimiza ndoto zao

  (GMT+08:00) 2018-03-20 16:32:25

  Mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China umefungwa leo hapa Beijing, ambapo rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuchaguliwa tena kwa muhula la pili, akimesema kuwa ataendelea kutekeleza majukumu aliyopewa na katiba, kuwa mhudumu wa wananchiraia na kupokea usimamizi wa watu. Amesisitiza kuwa enzi mpya ya ujamaa wenye umaalum wa Ckichina inamiliwa na wachina wote.

  Katika hotuba yake, rais Xi amewaambia watumishi wote wa vyombo vya serikali wakumbuke kuwa taifa lao ni China, bila kujali kuwa wanashika wadhifa gani, wanatakiwa kuweka kipaumbele maslahi ya wananchi, kuwahudumia wananchi kwa moyo wote na kufanya juhudi kuboresha maisha mazuri na yenye furaha ya watu. Anasema,

  "Kufanya kazi kama wananchi wanaunga mkono au la, kama wananchi wanakubali au la, na kama wananchi wanafurahi au la kuwa kigezo cha kimsingi cha kazi zote, kutilia mkazo kushughulikia maswalai ya maslahi wanayofuatillia zaidi wananchi na kuwawezesha wachina wote wafurahi na kujionea fahari na maendeleo ya taifa la China."

  Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China umepanga mpango wa kufanikisha ujenzi wa wa pande zote wa jamii yenye maisha bora, kuanzisha mchakato wa kujenga nchi ya kisasa ya ujamaa na kuleta ustawi mkubwa kwa taifa. Rais Xi amesema kufanya mpango huo kuwa hali halisi ni safari ndefu mpya, ambayo uzembe hauvumiliwi hata kidogo. Ametoa wito wa injini na hatua kabambe zaidi katika kuimarisha mageuzi katika sekta zote, kufungua zaidi mlango kwa nje, kufuata dira mpya ya maendeleo, kuhimiza maendeleo ya kiuchumi yenye ngazi ya juu na kukuza uchumi wenye ukuaji wa kasi ya kati hadi ya juu ili kuongeza uhai wa uchumi wa soko wa ujamaa. Pia amesisitiza umuhimu wa kuhimiza mchakato wa amani na umoja wa taifa.

  "Kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi, na kutimiza umoja kamili wa taifa ni matarajio ya pamoja ya wachina wote, pia kunahusu maslhimaslahi ya kimsingi ya taifa la China. Vitendo na njama zote zinazolenga kufarakisha taifa hakika zitashindwikana, kulaumiwa na wananchi na kuadhibitiwa na historia! Wachina wana nia imara, imani kamili na uwezo wa kutosha wa kuvunja shughuli zote za kufarakanisha taifa. Wananchi wa China na nchi yao tuna imani ya pamoja kuwa ardhi hata inchi moja haiwezi kutengwa kutoka China."

  Rais Xi Jinping pia amesema China haitajiendeleza kwa kukiuka maslahi ya nchi nyingine, na maendeleo ya China hayatakuwa tishio kwa nchi yoyote, na China kamwe haitatafuta umwamba wala kujipanuazi.

  "China itaendelea kulinda usawa na haki duniani, kuona kuwa watu wa nchi mbalimbali wanaweza kushauriana ili kutatua mambo ya dunia, na China haitalazimisha nchi nyingine kukubali maamuzi yake. China itaendelea kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuongeza mawasiliano na ushirikiano na nchi mbalimbali, na kufanya mageuzi na maendeleo ya China yawanufaishe wanabinadamu. China itaendelea kushiriki kwenye mageuzi na ujenzi wa usimamizi wa dunia, na kuchangia busara, mipango na nguvu ya China kwa dunia, ili kusaidia kujenga dunia iwe na amani ya kudumu, usalama wa jumla, ustawi wa pamoja, uwazi na ujumuishi, na mandhanimandhari nzuri."

  Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, rais Xi amesema Chama cha Kikomunisti cha China kinapaswa kushikilia misingi yakesimano wa uanzishwaji wake kwa ajili ya taifa na utekelezaji wa majukumu kwa ajili ya maslahi ya wananchi, na kuungana na kufanya juhudi pamoja na wananchi. (Sauti 6)

  "Chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, baada ya juhudi za miaka 70, Jamhuri ya Watu wa China imepiga hatua kubwa na kuwkaa katika mashariki ya Dunia kwa sura mpya. Enzi mpya inamilikiwa na wananchi wote, ambao wao ni mashuhuda, waanzishili na wajenzi wa enzi mpya. Kama wakishikamana na kufanya bidii juhudi kwa pamoja, hakuna nguvu yoyote inayoweza kuwazuia kutimiza ndoto zao."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako