• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Eneo la viwanda lka Mbale lavutia wawekezaji

    (GMT+08:00) 2018-03-20 18:15:51
    Eneo la Viwanda na Biashara lililozinduliwa hivi karibuni katika wilaya ya Mbale nchini Uganda imeanza kuvutia wadau kadhaa wakiwemo wafadhili.

    Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari huko Kampala, mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Orient Bwana Julius Kakeeto, alisema wamesaini mkataba na wawekezaji kutoka China.

    Alisema hatua hii inalenga kuimarisha ajenda ya Uganda kuelekea nchi yenye viwanda.

    Hata hivyo, wawekezaji hawatalazimishwa kujiunga na Benki ya Orient na watakuwa huru kutafuta fedha kutoka kwa taasisi nyingine.

    Eneo hilo la kiviwanda ambalo lilizinduliwa hivi karibuni na Rais Museveni linatarajiwa kuwa kitovu kikubwa cha viwanda katika eneo la mashariki mwa Uganda, na kuwa na zaidi ya viwanda 55 huku ajira 1,500 zikiundwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako