• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Ujenzi wa laini ya kusambaza umeme wa makaa Kenya kuanza

    (GMT+08:00) 2018-03-20 18:16:43
    Kampuni ya kujenga laini za kusambaza umeme nchini Kenya (Ketraco) inapanga kuanza kujenga laini ya umeme kutoka eneo la mradi wa kawi ya makaa ya Lamu.

    Ujenzi wa laini hiyo unatarajiwa kuanza mwezi Julai baada ya serikali kupata mkopo kutoka China.

    Mkurugenzi wa Ketraco Fernandes Barasa amesema laini hiyo ya kilomita 520 ya kilovolts 400 itagharimu dola milioni 220 (sawa na dola bilioni 22) na itakamilika baada ya miezi 36.

    Laini hiyo inatarajiwa kusafirisha megawati 960 za umeme kutoka kwa kituo cha Lamu hadi mjini Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako