• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN watoa wito wa kuwepo kwa utaratibu wa kuchunguza matumizi ya silaha ya kikemikali Syria

    (GMT+08:00) 2018-03-21 09:08:55

    Wajumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa wamelaani mwendelezo wa matumizi ya silaha za kikemikali nchini Syria na kusisitiza tena mwito wao wa kuwepo kwa utaratibu wa kuwawajibisha kisheria wanaojihusisha na uhalifu huo. Utaratibu wa pamoja wa kuchunguza matumizi ya silaha za kikemikali nchini Syria ulioidhinishwa na Baraza la usalama ulisimamisha kazi mwezi Novemba mwaka jana baada ya Russia kupiga kura ya turufu kupinga kurefusha muda wa idhini yake. Baraza la usalama limekutana kujadili suala hilo na kusisitiza kuwa matumizi ya silaha za kikemikali ni ukiukaji mbaya wa sheria za kimataifa, na kwamba makundi yote, serikali ya nchi yoyote au mtu yeyote binafsi anayejihusisha na uhalifu huo, anapaswa kufikishwa mbele ya sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako