• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya taifa ya Rwanda ya mpira wa wavu yaendelea na mazoezi

  (GMT+08:00) 2018-03-21 09:18:16

  Timu ya taifa ya Rwanda ya wanawake ya mpira wa wavu kwa viwanja vya ufukweni, imeendelea na kambi yake ya kujiandaa na mashindano ya jumuiya ya madola mwezi ujao nchini Australia.

  Timu hiyo inayoundwa na Charlotte Nzayisenga and Denyse Mutatsimpundu ilifuzu michuano hiyo kufuatia ubingwa ilioutwaa mwezi mei mwaka jana katika mashindano ya Msumbiji.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kocha mkuu wa timu hiyo, mazoezi yanafanyika mara mbili kwa siku katika uwanja wa amahoro na inatarajiwa kuondoka jumamosi kwenda Australia.

  Kwenye michuano ya jumuiya ya madola, Rwanda iko kundi C pamoja na timu za New Zealand, Vanuatu na Singapore.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako