• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa atoa mwito wa kuwepo kwa uvumilivu katika siku ya kupambana na ubaguzi wa rangi

    (GMT+08:00) 2018-03-21 09:18:45

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Geterres ametoa mwito wa kuwepo kwa uvumilivu wakati dunia ikiadhimisha siku ya kupambana na ubaguzi wa rangi.

    Akiongea kwenye mkutano wa baraza la umoja wa mataifa wa maadhimisho ya siku hiyo, Bw. Guterres amesema itikadi za siasa kali hazitakiwi kufanywa za kawaida na kuhalalishwa kwenye jamii. Jibu ni kutangaza na kuleta uvumilivu, kushirikisha watu na kuheshimu kuwepo kwa watu tofauti.

    Amesema licha ya maendeleo makubwa yaliyopatikana katika miaka 70 iliyopita baada ya kupitishwa kwa azimio la haki za binadamu, kutambua hazi zisizonyimika za binadamu, bado watu duniani wanaendelea kukabiliana na vikwazo mbalimbali na kunyimwa haki.

    Amesema bado kuna ubaguzi wa kijinsia na ukatili dhidi ya wanawake, kuna kuongezeka kwa haraka kwa chuki dhidi ya wageni, ubaguzi wa rangi na kukosa uvumilivu, na chuki dhidi ya wayahudi na waislamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako