• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msomi wa Uswisi asema hotuba aliyotoa rais Xi Jinping alipofunga mkutano wa Bunge imeonesha mwendelezo wa sera za uongozi

    (GMT+08:00) 2018-03-21 15:58:50

    Profesa Harro von Senger wa Chuo Kikuu cha de Fribourg nchini Uswisi amesema hotuba aliyoitoa rais Xi Jinping wa China alipofunga mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China imeonesha mwendelezo wa sera za uongozi za China

    Anasema, "Jambo linalovutia zaidi katika hotuba ya Rais Xi Jinping ni mwendelezo wake. Hili ni muhimu kwani China inafuata sera za siasa za muda mrefu na tulivu."

    Mwendelezo huo umeoneshwa kwenye marekebisho ya katiba, ambapo vipengele vya "kushikilia njia ya kujiendeleza kwa amani" "kushikilia mkakati wa kusaidiana, kunufaishana na kufungua mlango" na "kuhimiza kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja" vimeongezwa katika katiba. Profesa Fribourg anasema vipengele hivyo vimeweka bayana sera ya amani ya mambo ya nje inayofuata China siku zote.

    Anasema, "Naona vitu hivyo vinavyohusu mambo ya nje ya China vimeonesha kwa undani kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani za China, ni marekebisho mazuri."

    Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la China ulikamilika jana hapa Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako