• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Yemen akutana na mjumbe maalum mpya wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Yemen

    (GMT+08:00) 2018-03-21 16:37:09

    Rais Abdu-Rabbu Mansour Hadi wa Yemen amekutana na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Yemen Bw. Martin Griffiths nyumbani kwake mjini Riyadh, Saudi Arabia, ambapo wamejadiliana kuhusu kuanzisha tena mazungumzo ya amani ya pande mbalimbali za Yemen yanayoongozwa na Umoja huo.

    Rais Hadi amesema, serikali ya Yemen inaendelea kutoa wito wa amani nchini humo na kusisitiza huo ni msimamo wa kikanuni wa serikali na wajibu wa kimaadili kwa nchi. Pia amelaani kundi la Houthi kwa kukiuka makubaliano yaliyofikiwa na pande mbili na kutojali azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mazungumzo ya amani yaliyopita.

    Kwa upande wake, Bw. Griffiths amesema, atajitahidi kufanya upatanishi ili kutimiza amani ya Yemen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako