• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 26 wauawa na wengine 18 wajeruhiwa katika mlipuko uliotokea nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2018-03-21 17:51:54

    Watu 26 wameuawa na wengine 18 kujeruhiwa baada ya mtu mmoja kujilipua kwa bomu karibu na Chuo Kikuu cha Kabul nchini Afghanistan mapema leo.

    Ofisa mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema, huenda mtu huyo alitaka kujilipua kwenye Hekalu la Sakhi ambako maelfu ya watu walikusanyika kusherehekea mwaka mpya wa nchi hiyo, ila kutokana na ulinzi mkali alishindwa kufika eneo hilo hivyo kujilipua karibu na Chuo Kikuu hicho.

    Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan haijatoa tamko lolote kuhusiana na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako