• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Nigeria yathibitisha kuachiwa kwa baadhi ya wasichana waliotekwa nyara

    (GMT+08:00) 2018-03-21 18:00:50

    Serikali ya Nigeria leo imethibitisha kuwa, wanafunzi wa kike 76 kati ya 110 waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram kutoka chuo cha wasichana katika mji wa kaskazini mashariki wa Dapchi mwezi uliopita wameachiwa huru.

    Waziri wa habari na utamaduni wa Nigeria Bw. Lai Mohammed amesema kuwa, wasichana hao waliachiwa huru saa 9 alfajiri kwa saa za huko, na waliachwa bila sharti lolote.

    Mapema leo, msemaji wa rais wa Nigeria Garba Shehu amesema, wasichana hao wamepelekwa sehemu salama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako