• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kimataifa wa kuondoa umaskini wafunguliwa nchini Botswana

    (GMT+08:00) 2018-03-21 18:30:31

    Mkutano wa kimataifa wa kuondoa umaskini umeanza jana katika mji mkuu wa Botswana, Gaborone, ambapo maofisa na wataalamu kutoka nchi mbalimbali watabadilishana uzoefu na njia za kuondoa umaskini na kuimarisha ushirikiano husika kati ya nchi hizo.

    Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na serikali ya Boswana kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, na kauili mbiu yake ni kutoruhusu mtu yeyote kubaki nyuma katika mapambano ya kuondoa umaskini, kutengwa na kukosekana kwa usawa.

    Akihutubia mkutano huo, Rais Seretse Khama wa Boswana amesema kauli mbiu hiyo pia ni kanuni za mwongozo katika kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu yaliyotolewa nan chi mbalimbali mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako