• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa wakuu wa AU waanza

    (GMT+08:00) 2018-03-21 19:11:12

    Mkutano usio wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) umeanza leo mjini Kigali, Rwanda, ambapo viongozi hao wanatarajiwa kusaini makubaliano ya kuanzishwa kwa Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA).

    Akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja huo amesema, ajenda itakayojadiliwa ni kupitisha azimio la kuanzishwa kwa Eneo hilo. Amesema Itifaki kuhusu Uhuru wa Kutembea wa Watu na Azimio la Kigali ambalo linaonyesha umoja wa Afrika katika kusonga mbele, pia vimepangwa kupitishwa katika mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako