• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: AfDB imeidhinisha mkopo wa dola milioni 30 kusaidia uvumbuzi

    (GMT+08:00) 2018-03-21 19:43:00
    Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeidhinisha mkopo wa dola milioni 30 kusaidia kuanzishwa kwa hazina ya ufumbuzi ya Rwanda RIF.

    RIF inalega kukuza uchumi kupitia kwa uvumbuzi nchini Rwanda na eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ujumla.

    Kwa mujibu wa taarifa ya benki hiyo, fedha hizo zitatumika kuanzisha msingo wa uwekezaji na kufadhili biashara ndogo ndogo na za kati pamoja na kuendeleza uwezo wa ujasiriamali na mazingira ya uvumbuzi.

    Pia lengo la baadaye ni kukusanya dola milioni 100 moja kwa moja kutoka kwa wawekezaji wa Serikali na binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako