• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ajenda ya Rais John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda yaanza kutekelezwa

    (GMT+08:00) 2018-03-21 19:43:39
    Utekelezaji wa agizo la viwanda 100 kwa kila mkoa uliotolewa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Twala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ,Selemani Jafo,umefikia asilimia 49.4,viwanda 1,285 vikijengwa kati ya 2,600.

    Akizungumza katika kikao kazi cha kupitia bajeti ya Tamisemi na mikoa,Jafo alisema viwanda hivyo vimejengwa ndani ya miezi mitatu tangu kutolewa kwa agizo hilo.

    Alisema agizo hilo bado linaendelea kutekelezwa na kila mkoa unatakiwa kuhakikisha unajenga viwanda 100 kufikia Desemba 31 mwaka huu.

    Alibainisha kuwa kupitia wakuu wa mikoa,ajenda ya Rais John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda inatekelezwa na kuwataka waendelee kuitekeleza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako