• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa Utalii nchini Kenya,Najib Balala ataka wadau kutafuta vivutio vipya vya utalii

    (GMT+08:00) 2018-03-21 19:47:59

    Waziri wa utalii nchini Kenya Najib Balala amewataka wawekezaji katika sekta hiyo kuweka mikakati bora kukabiliana na dhana kuwa utalii nchini humo ni ghali ilhali huduma kwa watalii si bora.

    Sekta ya utalii nchini Kenya inaendelea kupata ushindani mkubwa kutoka vivutio vingine vya utalii katika soko la kimataifa kufuatia ukosefu wa mbinu za kisasa za kuvutia watalii.

    Akiongea mjini Mombasa,Waziri Balala alitaja changamoto nyingine kama kutegemea utalii sehemu kadhaa nchini.

    Alisema ipo haja kuwe na vivutio vipya vya utalii ili kuwavutia wageni nchini Kenya badala ya vile vya zamani hususan fuo za bahari na mbuga za wanyama.

    Aidha Balala alisema ni lazima kukabiliana na changamoto zilizopo ili kuinua sekta hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako