• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuadhimisha siku ya kimataifa ya misitu

  (GMT+08:00) 2018-03-21 19:55:38

  Leo ni siku ya misitu ya kimataifa.

  Wajumbe 200 kutoka baadhi ya nchi na mashirika ya kimataifa, na watu wa sekta mbalimbali za China wamepanda miti zaidi 700 kuadhimisha siku hiyo. Umoja wa Mataifa umetoa kauli mbiu ya siku ya misitu ya kimataifa ya mwaka huu kuwa ni "Misitu na miji endelevu".

  Habari nyingine zinasema, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limetoa ripoti ikisema, miji mingi inashughulikia kujenga mustakabali wenye maendeleo endelevu, na kumejitokeza mifano mingi ya maendeleo yasiyosababisha uchafuzi.

  Ripoti hiyo imesifu mpango wa mji wa Beijing wa kupanda miti ulioanza kutekelezwa mwaka 2012 na kusema, Beijing ikiwa ni mji wenye idadi kubwa ya watu na uchafuzi mkubwa wa hali ya hewa, eneo la misitu limechukua zaidi ya asilimia 25 ya maeneo ya tambarare mjini Beijing, na kujenga maeneo mengi ya burudani kwa wakazi wa mji huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako