• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Familia 140 zaondoa mji wa Harasta unaodhibitiwa na waasi katika Ghouta Mashariki, Syria

    (GMT+08:00) 2018-03-22 08:59:41

    Shirika la haki za binadamu nchini Syria limesema familia 140 zimeondoka mji wa Harasta unaodhibitiwa na waasi kwenye eneo la Ghouta mashariki, lililoko mashariki mwa mji mkuu Damascus, na kuelekea maeneo yanayodhibitiwa na serikali, baada ya ushoroba kufunguliwa kati ya maeneo hayo. Waziri wa maafikiano ya kitaifa wa Syria Bw. Ali Haidar amesema waasi wa kundi la Ahrar al-Sham wanaokalia mji wa Harasta pia wanatarajiwa kuondoka mji huo hivi karibuni, kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati yao na serikali ya Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako