• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yatoa siri kuhusu operesheni ya kuharibu vifaa vya nyuklia nchini Syria mwaka 2007

    (GMT+08:00) 2018-03-22 09:00:23

    Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu amepongeza vikosi vya usalama vya nchi hiyo kwa kufanikiwa kuharibu vifaa vya nyuklia vilivyoko eneo la al-Kubar nchini Syria kwenye operesheni maalumu iliyofanywa na vikosi hivyo mwaka 2007, baada ya nyaraka za siri kuhusu operesheni hiyo kuwekwa wazi jana. Bw. Netanyahu amesema serikali ya Israel, jeshi la Israel na shirika la ujasusi la Mossad wanastahili pongezi baada ya kufanikiwa kuizuia Syria kuendeleza uwezo wa kinyuklia, na kusisitiza kuwa Israel itaendelea na sera yake ya kuzuia maadui wake kupata silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako