• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la UN laongeza muda wa idhini ya jopo la wataalamu kuhusu Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-03-22 09:37:36

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha Azimio nambari 2407, ambalo linarefusha muda wa idhini ya jopo la wataalamu wanaoisaidia kamati ya vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini hadi tarehe 24 Aprili, 2019.

    Azimio hilo limepitishwa baada ya jopo hilo kuiwasilisha kwa Baraza la usalama la UN ripoti yake ya mwisho tarehe mosi mwezi huu. Azimio hilo linalenga kuzuia kuenea kwa silaha za kinyuklia, kikemikali na kibiolojia, pamoja na njia za kuzisafirisha silaha hizo, ambazo ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia.

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limefafanua madhumuni ya kurefusha muda wa idhini ya jopo hilo, na kutoa mwito kwa jopo hilo kuwasilisha ripoti ya kipindi cha kati tarehe 7 Septemba mwaka huu, na kuwasilisha ripoti ya mwisho kabla ya tarehe 14 Machi mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako