• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Vijana Tanzania yashinda mechi ya pili ya kirafiki

    (GMT+08:00) 2018-03-22 09:54:52

    TIMU ya soka taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imeendeleza umwamba katika kipindi cha hivi karibuni baada ya jana kufanikiwa kushinda kwa magoli 2-1dhidi ya Msumbiji katika mchezo wa kirafiki uliofanyika mjini Dar es Salaam.

    Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Tanzania baada ya Jumapili kuifunga Morocco bao 1-0 katika mchezo kama huo wa kirafiki.

    Katika mechi ya jana magoli ya Tanzania yalifungwa na Abdul Suleiman pamoja na Said Mussa Bakari, na goli la kufutia machozi la Msumbiji likifungwa na Belarmino Manhce kwa njia ya penati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako