• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lasisitiza umuhimu wa kuunganisha majeshi ya Libya

    (GMT+08:00) 2018-03-22 09:54:30

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza umuhimu wa kuunganisha majeshi ya Libya chini ya usimamizi wa kiraia, na kusisitiza kuwa hakuna utatuzi wa kijeshi wa mgogoro wa Libya.

    Mwenyekiti wa sasa wa baraza hilo ambaye ni mjumbe wa kudumu wa Uholanzi katika Umoja wa Mataifa Bibi Lise Gregoire-van Haaren, amesema wajumbe wa Baraza la Usalama wanaamini kuwa makubaliano ya kisiasa ya Libya yaliyosainiwa mwezi Desemba mwaka 2015, ni utaratibu pekee unaoweza kutekelezwa kukomesha mgogoro wa kisiasa nchini Libya kabla ya uchaguzi kufanyika na mpito wa kisiasa kumalizika.

    Amesema wajumbe wa baraza hilo wamewahimiza viongozi wa Libya kushiriki katika mazungumzo ya kiujenzi kwa msingi wa masikilizano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako