• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasichana 105 wa Nigeria waachiwa huru na Boko Haram

    (GMT+08:00) 2018-03-22 10:39:39

    Waziri wa habari na utamaduni wa Nigeria Bw. Lai Mohammed amesema mvulana mmoja na wasichana 105 waliotekwa na kundi la Boko Haram wameachiwa huru bila masharti na bila kutoa malipo yoyote, na hakuna mpiganaji wa kundi la Boko Haram aliyebadilishwa na wanafunzi hao.

    Bw. Mohammed amethibitisha kwamba watu hao wamekabidhiwa kwa serikali ya Nigeria.

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema Bw. Antonio Guterres amekaribisha kuachiwa kwa wasichana hao wakiwa salama, na kuhimiza serikali kuwafikisha wale waliohusika na tendo hilo mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako