• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa latakiwa kujibu kwa sauti moja suala la matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-03-22 18:18:26

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerudia tena wito wake kwa Baraza la Usalama la umoja huo kuonyesha mshikamano katika kutatua suala la matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu huyo Stephane Dujarric imesema, matumizi ya silaha za kemikali, katika mazingira yoyote, hayakubaliki, na pia kitu kingine kisichokubalika, ni kukaa kimya wakati silaha hizo zinapotumiwa.

    Amesema Bw. Guterres alikuwa akizungumzia kushindwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza muda wa mfumo wa pamoja wa uchunguzi wa umoja huo na Shirika la Kupiga Marufuku matumizi ya silaha za kemikali (OPCW) uliomalizika mwezi Novemba mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako