• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imekuwa nchi ya pili kwa kutoa maombi ya hataza duniani

    (GMT+08:00) 2018-03-22 18:56:42

    Shirika la kimataifa la hakimiliki ya ujuzilimetoa ripoti inayoonyesha kuwa, katika mwaka jana, China ilikuwa nchi ya pili kwa kuwasilisha maombi ya hataza chini ya mfumo wa mkataba wa ushirikiano wa hataza, ikiifuata Marekani.

    Ripoti hiyo imechambua hali ya nchi na makampuni yanayotoa maombi ya hataza zinazotumia huduma za shirika hilo. Kampuni za Huawei na ZTE za China ni kati ya makampuni yaliyotoa maombi mengi zaidi duniani.

    Mwaka 2017, Marekani ilitoa maombi elfu 56.6, ikifuatwa na China iliyotoa maombi elfu 48.9 na Japan maombi elfu 48.2. Kuanzia mwaka 2013, idadi ya maombi ya hataza ya China imeongezeka zaidi ya asilimia 10 kila mwaka. Ripoti hiyo imekadiria kuwa kutokana na hali hiyo, China inatarajia kuipita Marekani na kuwa nchi inayotoa maombi mengi zaidi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako