• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakimbizi 36 kutoka DRC wafariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2018-03-22 19:08:55

    Wakimbizi 36 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliotokea magharibi mwa Uganda mwezi uliopita.

    Taarifa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema, jumla ya kesi za ugonjwa huo zilizoripotiwa ni 1,747, kati yao 36 wamefariki tangu Februari 23 mwaka huu, wakati mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea kwenye kambi ya wakimbizi katika wilaya za kusini magharibi za Hoima na Kyegegwa.

    Jumatatu wiki hii, wagojwa wapya wa kipindupindu walipokewa katika kituo cha kutibu ugonjwa huo, wengi wao wakiwa wakimbizi wapya ambao wamekimbia mapigano kati ya makabila ya Lendu na Hema nchini DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako