• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Uganda na Kenya kuanzisha benki za mashinani 

    (GMT+08:00) 2018-03-22 19:30:43

    Kenya na Uganda zina mpango wa kuunda benki ya mashamba ambayo itakuwa mwongozo kwa wawekezaji wa kimaendeleo.

    Kenya imebaini kuwa kumekuwa na utata mkuu katika kupata vipande vya ardhi vya kushirikisha mikataba ya kimaelewano kati yake na wawekezaji, hivyo basi kuzindua harakati za kutambua ardhi yote ya umma na kuithibiti ndani ya benki hiyo.

    Kwa mujibu wa Katibu maalum wa Wizara ya Ardhi, Dkt Nicholas Muraguri, harakati hizo pia zitajumuisha kutathimini upya mashamba ambayo yanamilikiwa na tasaisi za serikali.

    Akiongea Jumatano afisini mwake wakati wa kuzindua jopo kazi ya kushirikisha uundaji wa benki hiyo, Dkt Muraguri alisema kuwa ardhi ya umma hapa nchini kwa kuwa haijajumuishwa pamoja na kulindwa na sheria za ugavi kwa miradi iliyotengewa, wanyakuzi na

    Alisema kuwa jopo hilo litashirikisha serikali za Kaunti, Tume ya Ardhi nchini (NLC) na maafisa wa Wizara ya Ardhi.

    Alisema kuwa benki hiyo itakuwa na takwimu kuhusu upana wa kila shamba, ufaafu wake wa kimaendeleo, bei na serikali ya Kaunti husika katika uratibu.

    Alisema kuwa mwekezaji akipatikana na ambaye anahitaji shamba, itakuwa rahisi kutambua ni wapi itapatikana na kwa bei gani na pia katika mtaala gani wa ujenzi.

    Nchini Uganda serikali imeshirikiana na Benki ya Duth ya Rabobank kutangaza mpango wa kuwaapatia wakulima fedha na kuwafungulia akaunti katika benki ili kujiendeleza na kupata mikopo.

    Robobank itatoa fursa hii kwa wakulima kupata mtaji na mkopo pamoja na kuwawezesha kupata pembejeo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako