• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Waajiri kushtakiwa na bodi ya mikopo

    (GMT+08:00) 2018-03-22 19:31:01

    Bodi ya mikopo nchini Tanzania imeapa kuwashtaki waajiri wasiosajili majina ya wafanyikazi wao wanaochukua mikopo katika benki.

    MkurugenziI Msaidizi wa Urejeshaji wa Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), Phidelis Joseph amesema kuanzia sasa waajiri wote ambao hawapeleki majina ya watumishi wanaodaiwa ndani ya siku 28, watachukuliwa hatua kali za kisheria.

    Akizungumza baada ya kutembelea waajiri watatu mjini hapa, alisema tatizo kubwa lililobainika katika siku mbili tangu kuanza operesheni mkoani Dodoma ni waajiri kutofuata matakwa ya sharia, ikiwa ni pamoja na kutowasilisha majina pindi wanapoajiri wafanyakazi wapya.

    Meneja wa Bodi ya Mikopo Kanda ya Kati, Octavilla Selemani amewataka waajiri kutoacha kutaka mikopo wanufaika ambao wanadaiwa deni kutokuwa sawa.

    Alizungumza katika operesheni ya kuwatembelea waajiri na waajiriwa mkoani hapa, alisema ni vema mwajiri akaendelea kukata deni wakati malalamiko ya ukubwa wa deni yakishughulikiwa.

    Aidha, Joseph alisema waajiriwa wengi wamekuwa wakilalamikia kuwa deni ni kubwa bila kujua kuwa kuchelewa kwao kulipa deni kunafanya deni hilo kuongezeka.

    Katika operesheni hiyo itakayofanyika wiki nzima, timu ya Bodi ya Mikopo imetembelea pia Chuo cha Sayansi ya Maendeleo ya Jamii, Shule ya Msingi ya St Ignatius na kiwanda cha Alko Vintages.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako