• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa Marekani wa kuitoza China ushuru wazusha wasiwasi wa vita ya biashara

    (GMT+08:00) 2018-03-23 08:46:52

    Rais Donald Trump wa Marekani ameamua kutoza ushuru wa dola bilioni 60 kwa bidhaa za China, licha ya maonyo makali kutoka kwa makundi ya kibiashara na wataalamu wa biashara. Ubalozi wa China nchini Marekani umeitaja hatua hiyo kama hatua wazi ya kujilinda kibiashara, na kusisitiza kuwa China inasikitishwa na kuipinga kithabiti. Rais Trump amemwagiza mwakilishi wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer kutoa orodha ya bidhaa za China zitakazotozwa ushuru ndani ya siku 15, na wizara ya fedha ya Marekani itapewa siku 60 kutoa mpango wa kuweka vizuizi dhidi ya uwekezaji wa China nchini Marekani. Wizara ya biashara ya China imesema China itachukua hatua zote za lazima kulinda haki na maslahi yake, na imeweka bayana msimamo wake kuwa inapinga kithabiti hatua za upande mmoja za kujilinda kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako