• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa atoa mwito wa kuwepo kwa mwamko kuhusu uhaba wa maji

    (GMT+08:00) 2018-03-23 08:55:26

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Antonio Guterres ametahadharisha kuwa kuongezeka kwa mahitaji ya maji na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa, kumefanya uhaba wa maji liwe jambo linalofuatiliwa sana.

    Akiongea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa kuhusu hatua za kupambana na uhaba wa maji uliofanyika kwenye baraza la umoja wa mataifa, Bw Guterres amesema mahitaji ya maji yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 40 katikati ya karne hii, na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea kushika kasi, yanaongeza shinikizo kwenye suala la usalama wa maji.

    Bw Guterres pia amesema asilimia 40 ya watu duniani kwa sasa wanasumbuliwa na uhaba wa maji, asilimia 80 ya maji taka yanaachwa kwenye mazingira bila kushughulikiwa, na asilimia 90 ya majanga yanatokana na maji.

    Amesema Umoja wa mataifa uko tayari kuzisaidia nchi kuhimiza mawasiliano ya kisera, kubadilishana uzoefu mzuri, kuinua mwamko na kuhimiza ushirikiano kukabiliana na changamoto za maji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako