• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza kufikiwa kwa makubaliano ya biashara huria barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-03-23 08:55:51

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres amesema kusainiwa kwa makubaliano ya kuanzisha biashara huria barani Afrika ni hatua muhimu kuelekea kufikia malengo ya maendeleo ya milenia, na kufanikisha ajenda ya amani na maendeleo kwa Afrika.

    Kwenye taarifa yake ya kupongeza kusainiwa kwa makubaliano hayo, Bw Guterres amesema umoja wa mataifa uko tayari kuliunga mkono bara la Afrika kutekeleza makubaliano hayo katika miezi ijayo.

    Kamishna wa biashara wa Umoja wa Afrika Bw Albert Muchanga amesema Umoja wa Afrika unapanga kuanza kutekeleza makubaliano hayo ndani ya mwaka mmoja, amesema utekelezaji huo utaanza baada ya nchi 22 kusaini makubaliano hayo.

    Wakati huo huo Kenya imesema kusainiwa kwa makubaliano hayo kuna mustakbali mzuri. Rais Uhuru Kenyatta amesema bara la Afrika sasa linaelekea kwenye mafanikio ya kiuchumi, baada ya viongozi kutambua kuwa nchi zitanufaika zaidi kwa kuungana kuliko kujitenga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako