• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yasaidia kulipa deni la kocha mkuu wa zamani wa timu ya taifa

    (GMT+08:00) 2018-03-23 08:57:28

    Hatimaye shirikisho la mpira wa miguu la Uganda FUFA kwa kushirikiana na serikali limelipa masalia ya malipo ya kocha mkuu wa zamani wa timu ya taifa Milutin Sredojevic 'Michu' ambaye alikatisha mkataba wake mwezi Julai mwaka jana kutokana na kutolipwa stahili zake.

    Kocha raia wa Serbia ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Orlando Pirates inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini, alivunja mkataba na Uganda kutokana na malimbikizo ya Mshahara yaliyofikia dola za kimarekani 64,000 sawa na shilingi milioni 230 za Uganda.

    Ili kulipa deni hilo serikali imechangia dola 20,000 na FUFA ikatoa dola 34,000 kwa ajili ya Michu, lakini habari zikieleza kuwa idara ya fedha ya FUFA imewalipa pia wachezaji na watendaji waliokuwa wanadai.

    Michu aliifundisha Uganda kwa mafanikio tangu mwaka 2013-2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako