• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa Msafara wa timu ya Kenya awasili Australia

    (GMT+08:00) 2018-03-23 08:58:13

    Licha ya kuwepo tetesi za mapungufu katika maandalizi ya timu ya Kenya inayokwenda kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola nchini Australia, hasa mivutano kuhusu malipo na masuala ya udhamini wa mavazi, mkuu wa msafara wa timu hiyo Barnabas Korir tayari amewasili katika mji wa mashindano wa Gold Coast.

    Korir aliyeambatana na baadhi ya wajumbe, ameeleza kuwa mazingira ya eneo la mashindano yapo salama, na ameanza kushirikiana na balozi wa Kenya nchini Australia kuandaa makazi ya wanamichezo.

    Kamati ya Olimpiki ya Kenya tayari imeendelea kushughulikia sintofahamu iliyojitokeza ili timu iweze kuwa tayari kwa mashindano hayo yanayoanza rasmi Aprili 4 na kumalizika Aprili 15.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako