• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hamilton na Vettel kuongeza ushindani msimu ujao ili kufikia rekodi ya Ubingwa mara tano

    (GMT+08:00) 2018-03-23 08:58:34

    Wakati msimu wa mashindano ya magari ya mwendokasi ukianza wikendi hii kwa mashindano ya Australia, wachambuzi wa masuala ya michezo hiyo wamesema ushindani utakuwa mkali baina ya madereva wawili, Lewis Hamilton wa Uingereza anayeitumikia timu ya Mercedes na Mjerumani Sebastian Vettel wa timu ya Ferrari.

    Ushindani huo unaelezwa kusababishwa na mambo matatu, moja kutokana na maandalizi binafsi waliyoyafanya, pili ni maboresho ya vifaa yaliyofanywa na timu zao na kubwa zaidi ni kutokana na kila mmoja kutaka kuingia katika rekodi ya ubingwa mara tano wa mashindano hayo kutokana na kila mmoja kuwahi kushinda taji hilo mara nne.

    Sebastian Vettel amewahi kushinda ubingwa huo mwaka 2010, 2011, 2012 na mwaka 2013, na Hamilton akiwahi kushinda mwaka 2008, 2014, 2015 na mwaka 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako