• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uongozi wa Bayern Munich wapendekeza kumwajiri kocha Mauricio Pochettino msimu ujao

    (GMT+08:00) 2018-03-23 08:59:20

    Bayern Munich inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani huenda ikamwajiri Muricio Pochettino kuwa kocha mpya wa timu hiyo msimu ujao kutokana habari kuwa kocha wa sasa Jupp Heyneckes ataachia ngazi mwishoni mwa msimu huu.

    Inadaiwa kuwa mkurugenzi wa michezo wa Bayern alifanya mazungumzo na Pochettino siku chache zilizopita na kisha kupendekeza jina lake kwa uongozi wa juu wa klabu hiyo.

    Kwa sasa Pochettino ambaye ni raia wa Argentina ana mkataba unaoisha mwaka 2021 wa kuifundisha Tottenham Hotspurs inayoshiriki ligi kuu Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako