• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa Afrika Mashariki wafanya juhudi kumaliza msukosuko wa wakimbizi wa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-03-23 09:16:25

    Mawaziri wa usalama kutoka kanda ya Afrika Mashariki wamesisitiza tena kuunga mkono hatua za uingiliaji zinazolenga kumaliza msukosuko wa wakimbizi nchini Somalia.

    Mawaziri kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD, wamekutana huko Nairobi kupitia mchakato wa kutekeleza mpango wa kikanda wa kutafuta utatuzi wa kudumu wa msukosuko wa wakimbizi nchini Somalia na kuahidi kuhamasisha raslimali na nguvu ya kisiasa ili kutimiza lengo hilo.

    Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya Bw. Fred Matiang'i amesisitiza kuwa fedha za kutosha, uhusiano wa kiwenzi na urafiki wa kisiasa ni umuhimu kwa kudumisha maendeleo yaliyopatikana katika kupunguza mateso ya wakimbizi wapatao laki 9 kutoka Somalia waliopo katika kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako