• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laeleza wasiwasi kuhusu hali ya kibinadamu DRC

    (GMT+08:00) 2018-03-23 09:16:42

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kibinadamu inayozidi kuwa mbaya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, na kusema katika baadhi ya maeneo hali hiyo imefikia kiwango cha kuwa janga.

    Baraza hilo limetoa taarifa ikieleza wasiwasi kuhusu idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani nchini DRC, ambayo imeongezeka zaidi ya maradufu kuliko ile ya mwaka jana na kufikia zaidi ya milioni 4.49, na wakimbizi laki 5.4 walioko nchini humo, pamoja na wengine zaidi ya laki 7.14 waliokimbilia nchi jirani.

    Baraza hilo limesisitiza haja ya kutatua suala la makundi ya kisilaha nchini humo na kusisitiza tena wito wa kuwepo kwa uchaguzi wazi, shirikishi na wenye kuaminika, ambao ni muhimu kwa amani na usalama wa kudumu nchini DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako