• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raundi ya kwanza ya mazungumzo kuhusu makubaliano ya biashara huria ya kipindi cha pili China na Korea Kusini yafanyika Seoul

    (GMT+08:00) 2018-03-23 09:56:43

    Raundi ya kwanza ya mazungumzo kuhusu kipindi cha pili cha Makubaliano ya biashara huria kati ya China na Korea Kusini imefanyika jana mjini Seoul, Korea Kusini.

    Naibu waziri wa biashara wa China ambaye pia ni naibu mwakilishi wa China kwenye mazungumzo ya biashara ya kimataifa Bw. Wang Shouwen na msaidizi wa waziri wa viwanda, biashara na raslimali wa Korea Kusini wameshiriki kwenye mazungumzo hayo.

    Pande zote mbili zimefurahishwa na utekelezaji wa makubaliano ya biashara huria ya kipindi cha kwanza. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, pande hizo mbili zitafanya mazungumzo kuhusu utoaji wa idhini ya kuingia katika soko la sekta za utoaji huduma na uwekezaji, pia zitafanya majadiliano kuamua majukumu ya mazungumzo hayo ya kipindi cha pili kuhusu makubaliano ya biashara huria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako