• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yaweka mikakati ya kuharakisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani

    (GMT+08:00) 2018-03-23 09:57:23
    Wataalamu wa mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika wamekutana mjini Nairobi ili kuweka mikakati ya kuharakisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

    Katibu wa Wizara ya mazingira na misitu ya Kenya Bw. Keriako Tobiko amesema, Wiki ya kwanza ya Hali ya Hewa ya Afrika itafanyika kati ya tarehe 9 na 13 Aprili mjini Nairobi.

    Amesema mkutano huo utakuwa jukwaa la kujadiliana kuhusu hatua za hali ya hewa katika bara la Afrika, na kuunga mkono utekelezaji wa hatua zinazohusika za nchi mbalimbali ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu.

    Bw. Tobiko pia amesema Kenya iko katika mchakato wa kuanzisha mfuko wa fedha wa mabadiliko ya hali ya hewa kwa mujibu wa makubaliano ya hali ya hewa ya mwaka 2016, ukiwa utaratibu wa kifedha wa kukabiliana na mabadiliko na hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako