• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yalaani ripoti kuhusu Sudan Kusini kutaka kubadilisha mahali pa mazungumzo ya amani

    (GMT+08:00) 2018-03-23 10:05:32

    Serikali ya Ethiopia imeshutumu ripoti kuwa serikali ya Sudan Kusini imeomba kubadilishwa kwa mahali pa mazungumzo ya amani, na kuitaja kuwa ni "habari feki".

    Ethiopia imekuwa kituo muhimu kwa mazungumzo ya amani kati ya rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na aliyekuwa makamu wake Riek Machar tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipolipuka mwezi Desemba mwaka 2013 nchini Sudan Kusini.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw Meles Alem amesema Ethiopia imepata barua kutoka serikali ya Sudan Kusini kuhusu matumaini yake kwa Ethiopia kuendelea kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini. Katika barua hiyo serikali ya Sudan Kusini pia imetoa shukrani kwa Norway, Marekani, Uingereza, China pamoja na nchi wanachama wa IGAD kwa uungaji mkono wao katika kuhimiza mchakato na mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako