• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Migogoro yasababisha ongezeko la njaa duniani

    (GMT+08:00) 2018-03-23 10:33:04
    Migogoro yasababisha ongezeko la njaa duniani

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema migogoro mingi duniani ndio chanzo kikuu cha ongezeko la njaa.

    Bw. Guterres amesema ripoti kuhusu msukosuko wa chakula duniani kwa mwaka huu inalenga kutoa tahadhari kuhusu ongezeko la idadi ya watu wanaosumbuliwa na njaa duniani.

    Bw. Guterres amesema kutokana na majanga ya hali ya hewa na migogoro, mwaka 2017 watu milioni 124 katika nchi 51 duniani walikabiliwa na msukosuko wa njaa, ni milioni 11 zaidi kuliko mwaka uliotangulia.

    Bw. Guterres amesema sasa ni wakati kwa hatua madhubuti kuchukuliwa ili kukidhi mahitaji ya wale wanaokumbwa na njaa na kuondoa migogoro ya nanma hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako