• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaharakisha ujenzi wa maeneo ya vielelezo vya uvumbuzi wa ajenda ya maendeleo endelevu ya taifa

  (GMT+08:00) 2018-03-23 17:41:49

  China inajenga maeneo ya vielelezo vya uvumbuzi wa ajenda ya maendeleo endelevu ya taifa katika miji mitatu ya Shenzhen, Taiyuan na Guilin, ambayo inataka kutafuta njia ya kukabiliana na changamoto katika maendeleo endelevu kutokana na umaalumu wao.

  Ili kuhimiza kutekeleza ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, China imeamua kujenga maeneo kumi ya vielelezo vya uvumbuzi wa ajenda ya maendeleo endelevu ya taifa kabla ya mwaka 2021, ili kutoa uzoefu kwa sehemu nyingine nchini China na hata nchi za nje. Naibu waziri wa sayansi na teknolojia wa China Bw. Xu Nanping amesema, hadi sasa miji mitatu imeidhinishwa kuanzisha eneo hilo. Anasema,

  "Kwa nyakati tofauti, miji na mikoa 15 ilitoa ombi la kuanzisha eneo hilo kwa wizara ya sayansi na teknolojia. Baada ya kufanya ukaguzi, tathmini na mikutano, tarehe 13 Februari baraza la serikali lilikubali miji ya Taiyuan, Guilin na Shenzhen kuanzisha eneo la vielelezo vya uvumbuzi wa ajenda ya maendeleo endelevu ya taifa."

  Miji hiyo ina hali tofauti, huku ikikabiliwa na changamoto tofauti katika kujipatia maendeleo endelevu. Ukiwa mji ulioendelea, mji wa Shenzhen unakabiliwa na matatizo ya ukosefu wa ardhi ya kutosha, uchafuzi wa mazingira, msongamano wa magari barabarani na ukosefu wa uwiano wa maendeleo. Meya wa mji huo amesema watazingatia miradi minne muhimu katika ujenzi wa eneo la vielelezo vya uvumbuzi wa ajenda ya maendeleo endelevu ya taifa. Anasema,

  "Miradi hiyo ni kuongeza ufanisi wa matumizi ya raslimali, kushughulikia vizuri uchafuzi wa mazingira, ujenzi wa mji yenye afya na njia za kisasa za kushughulikia mambo ya kijamii."

  Guilin ni mji wa utalii, changamoto zilizoukabili haswa ni uhifadhi wa mazingira. Katibu wa baraza la mji huo Bw. Zhao Leqin amesema, mji huo unatarajia kuweka mfano mzuri kwa sehemu nyingine zenye makabila mengi na mazingira dhaifu zilizoko magharibi na kati ya China, kupitia kujenga eneo la vielelezo vya uvumbuzi wa ajenda ya maendeleo endelevu ya taifa. Anasema,

  "Mji wa Guilin una mandhari nzuri, lakini mazingira yake ni dhaifu. Tunapaswa kutafuta njia mpya ya kuendeleza uchumi."

  Taiyuan ni mji wenye maliasili nyingi, ambao unakabiliwa na changamoto ya kurekebisha njia ya kujiendeleza, uchafuzi wa mazingira, na uwezo hafifu wa uvumbuzi. Meya wa mji huo Gen Yanbo anasema,

  "Tutapunguza utoaji wa makaa ya mawe, na kwa njia safi. Pia tutaboresha kiwango cha shughuli za makaa ya mawe, uyeyushaji wa madini na utengenezaji wa umeme, ili kuhifadhi mazingira."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako