• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaomba wawekezaji wa Israel kuwekeza nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-03-23 17:48:06

    Rais wa Tanzania Bw John Pombe Magufuli amewataka wawekezaji kutoka Israel kuwekeza kwa wingi nchini humo. Magufuli amesema Israel ni rafiki mkubwa wa miaka mingi hivo angependa kuona wawekezaji kutoka Israel wakiwekeza katika sekta ya Kilimo, madini na gesi. Akizungumza baada ya kufanya mazungumzo na waziri wa ulinzi wa Israel Bwana Avigdor Lieberman, Rais Magufuli amesema Tanzania ina dhamira ya dhati ya kukuza na kuimarisha ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Israel, na ametaka makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya kiuchumi yatiwe saini haraka ili utekelezaji wake uanze mara moja.

    Magufuli ameeleza dhamira yake ya kukuza utalii kwa kuwepo kwa ndege ya moja kwa moja kati ya viwanja vya ndege vya Dar es salaam, Kilimanjaro na Israel. Kwa upande wake, Avigdor Lieberman amemhakikishia Magufuli kuwa Israel imejipanga kuongeza uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania katika maeneo yote ya makubaliano pamoja na kusaidia kilimo na usindikaji wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako