• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijana Kenya watakiwa kutumia vizuri fursa zinazotolewa na serikali kujiendeleza kiuchumi

    (GMT+08:00) 2018-03-23 17:48:23

    Waziri wa Ugatuzi na maeneo kavu wa Kenya Bw Euegene Wamalwa amewataka vijana kutwaa nafasi zilizotolewa na serikali kujiimarisha kimapato. Amesema kuwa vijana ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo endelevu kwa hiyo wanahitaji kuhusishwa katika masuala makuu nchini Kenya. Wamalwa ameongeza kuwa inasikitisha kuona kuwa licha ya serikali kutoa shilingi bilioni 200 ni vijana wachache tu ambao wamejitokeza na kutumia huduma hiyo.Amesema fedha zilizochukuliwa sio zaidi ya shilingi bilioni 50 na kusisitiza kuwa vijana wanafaa kutumia nafasi hiyo kujinufaisha.Katika siku za hivi karibuni ukosefu wa ajira kwa vijana umesalia kuwa changamoto kubwa zaidi katika kufanikisha amani katika eneo zima la maziwa makuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako