• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya umeme kupungua kufuatia mvua kubwa Kenya

    (GMT+08:00) 2018-03-23 18:01:54

    Bei ya umeme inatarajiwa kupungua nchini Kenya kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha sehemu kadhaa nchini Kenya. Katibu katika wizara ya Kawi Bw Josphat Njoroge amesema huenda bei ya stima ikapungua baada ya bwawa la Masinga kujaa maji.Awali, maji katika bwawa la Masinga yalipungua kufuatia hali ya kiangazi.Bwawa hilo hufungwa kama maji yamepungua hadi miche mraba 1035. Hivi sasa maji katika bwawa hilo yamefikia miche mraba 1038.8. Februari 6 mwaka huu, waziri wa kawi Bw Alfred Keter alionya kuwa bwawa hilo huenda likafungwa kusiponyesha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako