• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuchukua hatua zote za lazima kulinda haki na maslahi yake

    (GMT+08:00) 2018-03-23 19:18:51

    Wizara ya biashara ya China leo imesema kuwa, China imefanya maandalizi ya kutosha kuchukua hatua zote za lazima kulinda haki na maslahi yake.

    Mkurugenzi wa idara ya sheria ya wizara ya biashara ya China Bw. Chen Fuli anasema, "Msimamo wa China wa kulinda haki na maslahi yake halali ni wazi na imara. Tumeonyesha mara nyingi msimamo wetu kuhusu uchunguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara ya Marekani, China haitaki vita ya biashara, pia haitachochea vita ya biashara. Lakini hatuogopi vita hiyo, pia hatuikwepi vita hiyo. Ukweli ni kwamba, China imefanya maandalizi ya kutosha, tutalinda kidhabiti haki na maslahi yetu halali. Tutafuatilia kwa karibu maendeleo husika kuhusu uchunguzi huo wa Marekani. Hatua husika za Marekai zikichukuliwa, China itazikabili. "

    Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying alikuwa na haya ya kusema, "Marekani inapuuza hali halisi ya China kuimarisha uhifadhi wa hakimiliki za ujuzi, kupuuza kanuni ya Shirika la Biashara Duniani, kupuuza wito kutoka sekta mbalimbali, kushikilia kuchukua hatua zake, hiki ni kitendo dhahiri cha upande mmoja na kujilinda kibiashara, China inakipinga kithabiti. Kitendo hiki cha Marekani hakisaidii maslahi ya China, hakisaidii maslahi ya Marekani, pia hakisaidii maslahi ya dunia, na ni mfano mbaya. Kwa vyovyote vile, China haitakubali haki na maslahi yake kuharibika, tumefanya maandalizi ya kutosha kulinda haki na maslahi yetu."

    Rais Donald Trump wa Marekani jana amesaini waraka wa kumbukumbu, na nchi hiyo itatoza ushuru zaidi kwa bidhaa zenye thamani ya dola za Kimareani bilioni 60 kutoka China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako