• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafikiria kuongeza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani

    (GMT+08:00) 2018-03-23 19:20:49

    China imetangaza leo kuwa inafikiria kuongeza ushuru zaidi kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani zenye thamani ya dola bilioni 3 za kimarekani ili kufidia hasara iliyosababishwa na ushuru unaotozwa na Marekani kwenye bidhaa za chuma na aluminium kutoka China.

    Hatua hii imekuja baada ya Marekani kuamua kuweka asilimia 25 ya ushuru kwenye bidhaa za chuma na asilimia 10 kwa bidhaa za aluminium, huku ikisamehe kodi hizo kwa nchi za Canada na Mexico.

    Tovuti ya Wizara ya Biashara ya China imetoa taarifa kuwa, uamuzi huo wa Marekani umekiuka mfumo wa biashara ya pande nyingi unaoongozwa na Shirika la Biashara Duniani, umeingilia mfumo wa biashara wa kimataifa, na umepingwa vikali na wajumbe wa Shirika hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako