• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China na spika wa bunge la umma la China wakutana rais wa Cameroon

    (GMT+08:00) 2018-03-23 20:46:12

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na spika wa bunge la umma la China Bw. Li Zhanshu leo hapa Beijing wamekutana na rais Paul Biya wa Cameroon.

    Bw. Li Keqiang amesema, China na nchi za Afrika ikiwemo Cameroon ni nchi zinazoendelea, zina maslahi ya pamoja ya maendeleo, na kwamba China itatoa msaada unaotakiwa kwa Cameroon bila sharti lolote la kisiasa. Kutokana na hali ya sasa, pande mbalimbali zinapaswa kulinda uhuru na urahisi wa biashara na uwekezaji, kufuata kanuni za soko na utaratibu wa kibiashara, na kupinga kujilinda kibiashara.

    Naye Bw. Li Zhanshu amesema, mabunge ya nchi hizo mbili yanapaswa kuungana mkono kisiasa, kuendelea kuboresha mazingira ya ushirikiano, kuimarisha msingi wa kiraia, ili watu wa pande hizo mbili wanufaike na ushirikiano huo.

    Kwa upande wake, rais Biya amesema, Cameroon inapongeza sera ya China kwa Afrika, na kushukuru China kuunga mkono na kusaidia maendeleo ya uchumi na jamii ya Cameroon. Amesema nchi yake itaendelea kuzidisha urafiki na ushirikiano kati ya pande hizo mbili, kuunga mkono mabunge ya nchi hizo mbili kuimarisha maingiliano, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuendeleza zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako