• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kudumisha utulivu wa biashara ya pande mbili

    (GMT+08:00) 2018-03-24 16:14:19

    Naibu waziri mkuu wa China Liu He amezungumza kwa simu na waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin, akihimiza juhudi halisi zifanywe ili kudumisha utulivu kwenye uhusiano wa kibiashara kati ya China na Marekani.

    Kwenye mazungumzo yao, Mnuchin ameufahamisha upande wa China kuhusu maendeleo mapya ya ripoti ya uchunguzi kwa mujibu wa kipengele namba 301 cha sheria ya biashara iliyotolewa na Marekani.

    Kwa upande wake, Liu amekumbusha kuwa ripoti hiyo imekiuka kanuni za sheria ya kimataifa na pia kuharibu maslahi ya China, ya Marekani na ya dunia nzima. Amesema China iko tayari na inaweza kulinda maslahi yake.

    Naye balozi wa China nchini Marekani amesema China inapinga vitendo vya kujilinda kibiashara na itapambana na vita yoyote ya biashara itakayoweza kutokea. Amesema hakika vita ya biashara itaharibu maisha ya watu wa tabaka la kati wa Marekani, kampuni za Marekani na soko la kifedha nchini humo. Ameongeza kuwa China haipendi kuingia katika vita ya biashara na nchi yoyote na inajaribu kuiepuka, lakini kama vita hiyo inalazimishwa, China itachukua hatua zote kuijibu.

    Wakati huohuo katibu mkuu wa Shirika la Biashara Duniani WTO Roberto Azevedo ametoa wito kwa nchi zote wanachama wajizuie na kufanya mazungumzo ya haraka ili kutatua masuala husika.

    Licha na maonyo kutoka kwa makundi ya biashara na wachumi nchini Marekani, rais Donald Trump Alhamisi alisaini kumbukumbu ya kuongeza ushuru wa hadi dola za kimarekani bilioni 60 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China na kuweka vizuizi kwa uwekezaji wa China nchini Marekani, hatua ambayo inahofiwa kusababisha nchi hizo mbili zinazochukua nafasi mbili za kwanza duniani kwa ukubwa wa uchumi kuingia kwenye vita ya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako