• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Haki za Binadamu la UM lapitisha azimio lililotolewa na China kuhusu ushirikiano wa kunufaishana

    (GMT+08:00) 2018-03-24 18:08:02

    Mkutano wa 37 wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa umepitisha azimio lililotolewa na China la kuhimiza ushirikiano wa kunufaika pamoja kwenye sekta ya haki za kibinadamu.

    Azimio hilo limetambua umuhimu wa nchi mbalimbali kufanya juhudi kwa pamoja, ili kujenga uhusiano wa kimataifa wenye kuheshimiana, haki na usawa, kunufaishana na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Azimio hilo pia linataka kazi za Baraza la Haki za Binadamu kuongozwa kwa kufuata kanuni za kimataifa, misingi ya uadilifu, kutopendelea na bila kubagua, kusaidia uendeshaji wa majadiliano na kuboresha ushirikiano wa kimataifa unaolenga kuhimiza uimarishwaji na ulinzi wa haki zote za kibinadamu, ikiwemo haki ya kupata maendeleo.

    Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Yu Jianhua amesema, muswada wa azimio hilo ulitolewa na China kwa kufuata matumaini ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa na mwelekeo wa maendeleo ya sasa, ni mchango wa nchi wanachama ikiwemo China kwenye usimamizi wa haki za kibinadamu duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako