• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sehemu ya kwanza ya waasi yaondoka Ghouta Mashariki, Syria

    (GMT+08:00) 2018-03-25 16:29:22

    Sehemu ya kwanza ya waasi wa kundi la Failaq al-Rahman na ndugu zao imeondoka kwenye eneo la Ghouta Mashariki nchini Syria.

    Msafara huo wenye mabasi 17 yakisafirisha waasi 981 na familia zao umelekea kwenye maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mkoa wa Idlib, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, kufuatia makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni na serikali ya Syria chini ya upatanishi wa Russia. Kabla ya kuhama kwa waasi, jumla ya watu wanane waliotekwa nyara na waasi katika Ghouta Mashariki waliachiliwa huru, ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa kabla ya hapo.

    Kwa mujibu wa makubaliano hayo, waasi 7,000 na wanafamilia wao wataondoka maeneo ya Jobar, Zamalka, Arbeen na Ayn Tarma katika Ghouta Mashariki na makubaliano hayo yanahusisha makundi makuu ya waasi yanayodhibiti maeneo hayo likiwemo kundi la Failaq al-Rahman na kundi la Nusra Front lenye uhusiano na al-Qaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako